Wahenga wanasema elimu haina mwisho,inapotokea fursa hupaswi kuiacha kwani hiyo inakuwa na moja ya kujiongezea maarifa. Na Hobokela Lwinga Naibu waziri wa utamaduni Sanaa na michezo Mhe. HAMIS MWINJUMA amesema lugha ya Kiswahili ni kiungo muhimu cha mawasiliano miongoni mwa watu wanaofanya shughuli za uchumi wa buluu katika nchi yetu na Nchi nyingine. Mhe.Mwinjuma ameyasema hayo leo wakati akifunga kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani lililofanyika jijini Mbeya. Aidha Mhe.Mwinjuma amevitaka vyombo vya habari kutumia misamiati inayofaa katika kutoa habari ili wasikilizaji wajifunze Kiswahili fasaha ili kiendelee kuenea Zaidi ulimwenguni.
Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Bi.Consolata Mushi amesema taifa linatekeleza mkakati wa taifa wa kubidhaisha Kiswahili ambao ulianza mwaka 2022 na utaitimishwa rasmi mwaka 2032. Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Batenga amewata watanzania kuendelea kuenzi, kukikuza na kukibidhaisha kiswahili kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza ustawi wa jamii na uchumi. Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wameeleza namna walivyo nufaika na mafunzo hayo. Kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani lilianza tarehe 18 march 2024 na kufungwa ijumaahii ya march 22 likiwa na kauli mbiu:Tasnia ya habari na fursa za ubidhaishaji kiswahili duniani.